Posts

Showing posts from April, 2023

96 - Mali Yako Sasa

 96 - Mali Yako Sasa "We Give THee But Thine Own" 1. Mali yako sasa, Bwana, tutatoa; Hatuna yaliyo yetu, Yote ni vipaji. 2. Sisi watumishi, Twaungama deni; Tungeirudisha kwake, Iliyo ya Bwana. 3. Utusaidie, Upendo kujua, Kwa ajili yao wote Walio gizani. 4. Neno tumaini Na tegemea: Kwamba lote tufanyalo, Tulifanye kwako. (Amina)

97 - Sioshwi Dhambi Zangu?

97 - Sioshwi Dhambi Zangu? "What Can Wash Away My Sin?" 1. Sioshwi dhambi zangu? Bila damu yake Yesu, Hapendezewi Mungu? Bila damu yake Yesu. Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa ila Damu yake Yesu. 2. La kunisafi sina, Ila Damu yake Yesu. Wala udhuru tena, ila Damu yake Yesu. 3. Sipati patanishwa, Bila damu yake Yesu, Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu. 4. Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu, Wema wala amani Bila damu yake Yesu. 5. Yashinda ulimwengu, Iyo, damu yake Yesu, Na kutufikisha juu, Iyo, damu yake Yesu.   (Amina)

98 - Nilikupa Wewe

98 - Nilikupa Wewe "I Gave My Life For Thee" 1. Nilikupa wewe, damu ya moyoni, Ili wokolewe, winuke ufuni. Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini? Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini? 2. Nilikupa miaka yangu duniani; Upate inuka, kuishi mbinguni. 3. Nimekuiletea, huku duniani; Pendo na wokovu, zatoka mbinguni. 4. Nipe siku zako, udumu mwangani; Na taabu yako, wingie rahani. Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanweli. Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanweli. (Amina)

99 - Twende Kwa Yesu

99 - Twende Kwa Yesu "Come To The Saviour" 1. Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue Imo Chuoni na mwenyewe, Hapa asema, njoo! Na furaha tutaiyona, Mioyo ikitakata sana, Kwako Mwokozi kuonana, Na milele kukaa. 2. "Wana na waje," atwambia, Furahini kwa kusikia; Ndiye Mwokozi wetu hasa, Na tumtii, njoni. 3. Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zitwitapo, Ewe kijana, njoo. (Amina)

100 - Kuwatafuta Wasioweza

  100 - Kuwatafuta Wasioweza "Seeking The Lost" 1. Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, "Njooni kwangu, nawapenda". Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute Wapotevu (wapotevu) wageuke,  Waingie (Waingie) Katika zizi La Mwokozi (La Mwokozi) Yesu Kristo 2. Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu; Kuwaongoza, wapate wote uzima ule wa milele. 3. Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito; Kuwainua waangukao, waletwe kwake yesu Njia. (Amina)

101 - Yesu Akwita

 101 - Yesu Akwita "Jesus Is Tenderly Calling Today' 1. Yesu Akwita, Akwita wewe, Uje leo, uje leo, Kwani kusita, akwita wewe, Unatanga upeo. Msiskie, msikie, Yesu akwita, ujitoe moyo sasa. 2. Waiochoka, na wapumzike, Uje leo, uje leo, Wenye mizigo, wenye huzuni, Wapate mapumziko. 3. Anakungoja uliye yote, Uje leo, uje leo, Uliyekosa, usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo. 4. Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo, Wafurahi waaminio; Amka, upesi, Njoo. (Amina)

102 - Mlango Pa Moyo

  102 - Mlango Pa Moyo "There's A Stranger At The Door" 1. Mlangoni pa moyo; Mgeni! (Amesimama)  Amesimama pale, Mgeni! (Amesimama)  Umkaribishe sasa,  Umkaribishe Mwana  Wa Baba wa upendo: Mgeni! (Umkaribishe)  2. Moyo wako kwa Bwana, Fungua. (Fungulieni)  Asikuache mbali, Fungua. (Fungulieni)  Umkubali Rafiki,  Roho atafariji  Naye atakutunza: Fungua. (Fungukieni)  3. Usikie sauti Ya Bwana. (Uisikie)  Uyachague mambo Ya Bwana. (Mambo ya Bwana)  Ufungue mlango,  Usimwambie bado:  Jina lake tumai---- Yu Bwana. (Jina la Bwana)  4. Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)  Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)  Uzuri utavikwa  Dhambi ataondoa,  Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni) (Amina)

103 - Njoni Kwangu

103 - Njoni Kwangu "Softly And Tenderly" 1. Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami;  Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.  "Njoni kwangu, Mliochoka, njoni:  Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, "uje kwangu"  2. Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi;  Usidharau wema na huruma, Huruma kwetu sisi.  3. Siku za maisha hupota hima, Hupita kwako, kwangu;  Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.  4. Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu;  Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu. (Amina)

104 - Yesu Aliniita , Njoo

 104 - Yesu Aliniita , Njoo " I Heard The Voice Of Jesus Say" 1. Yesu aliniita, "Njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze kituani mwangu." Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka; Nikapata kwake raha na furaha. 2. Yesu aliniita, "Njoo, Kwangu kuna maki: Maji ya Uzima, bure, unywe uwe hai." Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa: Naishi kwake na kiu kamwe sina tena. 3. Yesu aliniita, "Njoo, Dunia i giza, Ukinitazama, nuru `takungarizia." Nilikwenda kwake mara, Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga safarini mwangu. (Amina)

105 - Mchungaji Mpenzi

 105 - Mchungaji Mpenzi "Jesus The Loving Shepherd" 1. Mchungaji mpenzi hukuita uje Katika zizi lake panapo salama; Akina wanawake, waume vijana, Yesu aliye kweli, huwaita kwake.   Huita kwa moyo wa huruma, "Uliyepotea uje kwangu" Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu Mchunga. 2. Akatoa maisha kwa ajili yetu; Ataka wapotevu waje kwake sasa; Tusijihatirishe; Kwake tu salama; Sikia wito wake, Mchungaji wetu. 3. Tusikawie tena, adui Shetani, Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu; Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu, Tuingie zizini, panapo nafasi. (Amina)

106 - Huna Kitu Kwa Yesu?

 106 - Huna Kitu Kwa Yesu? "Crowded Is Your Heart" 1. Ukitafuta mali, Huna wasaa kwa Yesu? Kwa matendo ya haki Huna wasaa kwa Yesu? Anasa za dunia, Mambo yako ya raha Haya unatafuta; Huna wasaa kwa Yesu?  2. Mambo yanakusonga: Kwakehuna nafasi?  Watekwa na dunia, Kwake huna nafasi? Humwona m-langoni, Anapopiga hodi? Daima hukusihi: Kwake huna nafasi?  3. Sa-a ni za thamani, Kwake hamnayo kazi Wala hamfanyi bidii, Kwake hamnayo kazi?  Hamkufikia kwao Waliomo shimoni Na waliopotea? Kwake hamnayo kazi?  4. Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu? Mikono I mitupu, Huna tunda kwa Yesu? Huna chembe kwa ghala Kazi yako kulipa;  Wala huna furaha Unapomwona Yesu? (Amina)

107 - Sauti Ni Yake Bwana

  107 - Sauti Ni Yake Bwana "Hark The Voice Of Jesus" 1. Sauti ni yake Bwana, "Kwenda nani tayari?" Mavuno yanakawia, Nani atayavuna? Kwa kudumu anaita, Zawadi atatoa; Nani atakayejibu, "Nipo Bwana nitume." 2. Kama huwezi safari, Hata nchi za mbali, Pana watu karibuni, Wasiomjua Yesu; Kama huwezi kusema, Jinsi ya malaika, Waweza kuutangaza, Upendo wa Mwokozi. 3. Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoni, Ukiwatolea watu, Nafasi ya uzima; Kwa sala na kwa sadaka, Watoa msaada, Kama Harun mwaminifu, Kuinua mikono. 4. Roho za watu zikifa, Bwana akikuita, Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu". Kwa furaha anza kazi, Ile aliyokupa, Ukajibu mara moja, "Nipo Bwana nitume". (Amina)

108 - Tumesikia Mbiu

 108 - Tumesikia Mbiu "We Have Heard" 1. Tumesikia mbiu: Yesu huokoa; Utangazeni kote, Yesu huokoa. Tiini amri hiyo: nchini baharini. Enezeni mbiu hii: Yesu huokoa. 2. Imba nawe askari: Yesu huokoa Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa. Imbeni wenye shida, unapoumwa moyo, Na kaburini imba: Yesu huokoa.  3. Mawimbini uenee. Yesu huokoa; Wenye dhambi jueni: Yesu huokoa; Visiwa na viimbie, vilindi itikeni, Na nchi shangilie: Yesu huokoa.  4. Upepo utangaze: Yesu huokoa; Mataifa yashangaa: Yesu huokoa. Milimani, bondeni, sauti isikike Ya wimbo wa washindi: Yesu huokoa. (Amina)

109 - Anisikiaye

109 - Anisikiaye "Whosoever Heareth" 1. Anisikiaye, aliye yote, sana litangae, wajue wote, Duniani kote neno wapate, atakaye na aje! Ni "atakaye," ni "atakaye";   Pwani hata bara, na litangae:  Ni Baba mpenzi alinganaye atakaye na aje . 2. Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema;  Ndimi Njia, kweli, ndimi uzima: atakaye na aje! 3. Atakaye aje, ndiyo ahadi; atakaye hiyo haitarudi!  Atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.    (Amina)

110 - Mlango Wazi

110 - Mlango Wazi "There Is A Gate" 1. Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:  Yesu ameufungua Na hakuna kufunga   Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?  Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu? 2. Mlango hukaa wazi Watu waokolewe:  Maskini na matajiri Wa mataifa yote. 3. Maadam mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;  Msalaba ukubali - Amana ya upendo. 4. Msalaba tutabeba Daima, na furaha!  `Pendo wa Yesu hushinda. Tunainama kwake!   (Amina)

111 - Tabibu Mkuu

 111 - Tabibu Mkuu "The Great Physician" 1. Tabibu mkuu huyu, Yesu mwenye huruma Atuletaye faraja: Yesu, Mwokozi wetu. Imbeni, Malaika, SIfa za Bwana wetu: Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana. 2. Mwana Kondo-o msifuni Mwokozi;  Hatia zote na dhambi, Huziondoa Yesu. 3. Hakuna jina jingine, Linalofa-a sifa;  A-u kutufurahisha, Isipokuwa lake. 4. Naye atakapokuja, Na utukufu wake; Tutafurahi milele, Kuka-a kwake Bwana. (Amina)

112 - Wewe Umechoka Sana?

  112 - Wewe Umechoka Sana? "Art Thou Weary" 1. Wewe umechoka sana? Wataka raha?  Kwake Yesu utapata - Msaada. 2. Alama anazo Yeye? Sana! Makovu  Ya mikono, na miguu, Na mbavu. 3. Naye amevikwa taji Kichwani Mwake?  Taji, kweli, alivikwa - Miiba! 4. Huku nikimfuata, Nipate nini? Maonjo nje, na ndani Amani. 5. Kwamba namwandama yeye, Mwisho ni nini?  Kurithi furaha naye - Milele. (Amina)

113 - Bubujiko

  113 - Bubujiko "There Is A Fountain" 1. Damu imebubujika, Ni ya Imanweli,  Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli. 2. Ilimpa kushukuru Mwivi mautini;  Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.   3. Kondo-o wa kuuawa, Damu ina nguvu,  Wako wote kuokoa Kwa utimilivu.   4. Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale,  Nimeimba sifa zako, `taimba milele. 5. Bwana, umenikirimu Nisiyestahili  Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli. 6. Nikubali kukwimbia Mbinguni milele.  Mungu nitamsifia Jina lako pweke. (Amina)

114 - Yesu Nataka Kutakaswa Sana

114 - Yesu Nataka Kutakaswa Sana "Lord Jesus, I Long To Be Perfectly Whole" 1. Yesu Mwokozi ili nitakaswe, nataka moyo uwe enzi yako. Ukiangushe kilichoinuka unioshe sasa niwe mweupe. Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi. 2. Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai. Najitoa kwako, na moyo, vyote; unioshe sana niwe mweupe. 3. Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakuongojea miguuni pako, Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.   (Amina)

115 - Naendea Msalaba

  115 - Naendea Msalaba "Am Coming To The Cross" 1. Naendea msalaba, Ni mnyonge, mpofu,  Yapitayo naacha nipe msalaba tu. Nakutumaini tu, ewe Mwana wa Mungu;  Nainamia kwako; niponye sasa, Bwana. 2. Nakulilia sana: nalemewa na dhambi;  Pole Yesu asema: "Nitazifuta zote." 3. Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,  Roho yangu na mwili viwe vyako milele. 4. Kwa damu yake sasa amenivuta sana,  Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi. (Amina)

116 - Moyo Safi

 116 - Moyo Safi "One Thing Of Thee Lord I Desire" 1. Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka,  Kwa moto au kwa maji unisafishe kabisa. Unisafishe Mwokozi ndani, na nje, kwa moto  Utakavyo: ili dhambi ife kwangu, ife kwangu. 2. Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa;  Lakini moyo safi ni, bora kwangu, bora kwangu! 3. Mpaka moyo ni safi siwezi kuyafahamu  Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu. (Amina)

117 - Wamwendea Yesu ?

 117 - Wamwendea Yesu ? "Have You Been To Jesus?" 1. Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya Kondoo?  Je, neema yake yatumwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?  Kuoshwa kwa damu Itutakasayo ya Kondoo? Ziwe safi nguo nyeupe sana; Waoshwa kwa damu ya Kondoo?  2. Wamwandama daima Mkombozi. Waoshwa kwa damu ya Kondoo? Yako kwa Msulubiwa  mavazi? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?  3. Atakapokuja Bwana-arusi Uwe safi katika damu!  Yafae kwenda mbinguni mavazi: Yaoshwa kwa damu ya Kondoo? 4. Yatupwe yalipo na takataka; Uoshwe kwa damu ya Kondoo: Huoni kijito chatiririka Uoshwe kwa damu ya Kondoo?  (Amina)

118 - Nilipotoka Kabisa

118 - Nilipotoka Kabisa "I've Wondered Far Away " 1.                  Nilipotoka kabisa, sasa narudi; Nikakawia dhambini, Bwana narudi. Narudi nyumbani: daima kwako.  Kwa upendo nipokee: Naja nyumbani. 2. Nikasusurika sana, sasa narudi;  Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi. 3. Nimechoka maovuni, sasa narudi;  Pendo lako lanivuta, Bwana narudi. 4. Ndilo tumaini langu, sasa narudi;  Yesu alinifilia, Bwana narudi. 5.   Damu yake yanitosha, sasa narudi;  Unioshe kenyekenye, Bwana narudi.   (Amina)

119 - Alilipa Bei

119 - Alilipa Bei "I Hear The Saviour Say" 1. Yesu anasema, "Wewe huna nguvu, Kesha ukaombe, Na uje, Mwanagu." Alilipa bei, Nawiwa naye; Dhambi ilitia waa, Aliiondoa. 2. Bwana, nimeona, Uwezo wako tu, Waweza `takasa Mioyo michafu. 3. Sina kitu chema, kudai neema, Hivi nitafua, Mavazi kwa damu. 4. Ninaposimama, Juu ya mawingu, Taji nitaweka, Miguuni pa Yesu.  (Amina)

120 - Msalaba Wa Yesu

  120 - Msalaba Wa Yesu "Jesus Keep Me Near The Cross" 1. Msalaba wa Yesu, Nikae karibu;  Pale pana chemchemi Yakuponya dhambi. Pale msalaba Msalaba wake,  Huo ni sifa yangu Kwa maisha yote. 2. Karibu msalaba Nalitetemeka, Pendo likaniona Likanirehemu. 3. Unikumbushe, Yesu. Nikuone pale:  Niupate upendo Na kuvutwa nao. 4. Karibu msalaba, Kwa kutegemea,  Kukesha na kungoja, Nitakaa pale. (Amina)