104 - Yesu Aliniita , Njoo

 104 - Yesu Aliniita , Njoo
" I Heard The Voice Of Jesus Say"

1.

Yesu aliniita, "Njoo, Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze kituani mwangu."
Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha na furaha.

2.

Yesu aliniita, "Njoo, Kwangu kuna maki:
Maji ya Uzima, bure, unywe uwe hai."
Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa:
Naishi kwake na kiu kamwe sina tena.

3.

Yesu aliniita, "Njoo, Dunia i giza,
Ukinitazama, nuru `takungarizia."
Nilikwenda kwake mara, Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga safarini mwangu.

(Amina)

Comments